Swahili
Je, unahitaji usaidizi katika lugha yako? Ita 1800 512 451 na omba mkalimani.
Mentoring for Growth (M4G) inatoa kwa biashara zinazostahiki ufikiaji bila malipo kwa wataalam wa kujitolea wa biashara ambao hutoa maarifa, chaguo na mapendekezo yanayohusiana na changamoto na fursa unazopitia katika biashara yako.
M4G programu inasaidia biashara katika Queensland ili kukua na kufanikiwa katika mazingira ya sasa ya biashara.
Programu za M4G zinajumuisha:
- Ushauri kwa vikao vya Ukuaji
- Ushauri kwa Uwekezaji
- Ushauri kwa Maeneo husika
- Ushauri kwa ajili ya kuuza nje
- Ushauri kwa Ahueni.
Unaposhiriki katika programu M4G, Serikali ya Queensland inalinganisha utaalamu na uzoefu wa washauri wake na changamoto ya biashara au fursa uliyotambua.
Washauri huchaguliwa kutoka kundi kubwa la Queensland- lenye zaidi ya washauri 300 waliojiandikisha. Washauri wote wana utaalamu na uzoefu katika kufundisha na/au kuendeleza biashara.
Mentoring for Growth kwa sasa inatolewa mtandaoni pekee. Mpango huo unapatikana kwa biashara zote kuzunguka Queensland.
Pia angalia...
- Jifunze jinsi ya kuandikisha biashara yako kwenye kikao cha Mentoring for Growth.
- Soma kuhusu kujiandikisha kama mshauri wa Mentoring for Growth.